Kuhusu Tukio
Kwanini Kansa ya Kizazi
Kulingana na taarifa zilizopatikana kutoka kituo cha kansa cha Ocean Road kuna visa vipya 42,060 vya wagonjwa wa kansa Tanzania ambapo asilimia kati ya 65 mpaka 70 ya wagonjwa hao ni wanawake. Kansa ya kizazi inaongoza kwa asilimia zaidi ya 35 ya visa vay kansa. Umri wa wagonjwa ni kuanzia miaka 18 mpaka miaka 80 ambapo wagpnjwa wengi ni miaka ya 40 na HPV ndiyo chanzo kikuu kwa asilimia 99.9 ya visa vote. Kansa ya kizazi inaweza kuepukika lakini ni chanzo kikubwa cha vifo kwa wanawake nchini Tanzania. Pia, asilimia zaidi ya 80 ya kesi zinazogundulika ni huwa katika hali ya hatari zaidi kwa sababu ya ukosefu wa elimu ya afya, vipimo na tiba ya kansa.