Menu

NBC Events Portal

Kujisajili, fungua ukurasa ya NBC Marathon na kisha fuata maelekezo.

Kuhusu

about

Tunayo furaha kuandaa mbio hizi za nyika ambazo zinatarajiwa kufanyika siku ya Jumapili tarehe 22 mwezi wa Novemba mwaka 2020. Mbio hizi zinatarajia kuwakaribisha washiriki 3000 kutoka katika kada ya wanariadha wenye uzoefu na wale wanaochipukia kona mbalimbali za nchi. Mbio hizi zitahusisha umbali wa Kilomita 42, Kilomita 21, Kilomita 10 na Kilomita 5. Nia na dhumuni la kuandaa mbio hizi ni kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi nchini. Saratani hii ni hatari sana kwa wanawake ambapo zaidi ya 85% ya vifo vyake vinatokea kwenye nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Lengo kuu la mbio hizi ni kusaidia kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na saratani hii. Katika kufanikisha hili tunashirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyo chini ya Wizara ya Afya. Vile vile katika kufanikisha hili tunashirikiana na Riadha Tanzania ambao ndio wenye dhamana ya kuratibu na kusajili mbio hapa nchini zikiwemo zile za nyika.

Menejimenti

NBC BANK Plc