NBC Events Portal

03

Kuhusu Mbio za NBC
Kuhusu Tukio

Tunayo furaha kuandaa mbio hizi za nyika ambazo zinatarajiwa kufanyika siku ya Jumapili tarehe 22 mwezi wa Novemba mwaka 2020. Mbio hizi zinatarajia kuwakaribisha washiriki 3000 kutoka katika kada ya wanariadha wenye uzoefu na wale wanaochipukia kona mbalimbali za nchi. Mbio hizi zitahusisha umbali wa Kilomita 42, Kilomita 21, Kilomita 10 na Kilomita 5. Nia na dhumuni la kuandaa mbio hizi ni kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi nchini. Saratani hii ni hatari sana kwa wanawake ambapo zaidi ya 85% ya vifo vyake vinatokea kwenye nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Lengo kuu la mbio hizi ni kusaidia kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na saratani hii. Katika kufanikisha hili tunashirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyo chini ya Wizara ya Afya. Vile vile katika kufanikisha hili tunashirikiana na Riadha Tanzania ambao ndio wenye dhamana ya kuratibu na kusajili mbio hapa nchini zikiwemo zile za nyika.

0

Siku

0

Saa

0

Dakika

0

Sekunde
Sajili

Mazoezi ya Kansa ya kizaki na NBC Marathon.

Angalia Video

Chagua Tiketi

Event details

Kwanini Kansa ya Kizazi

Kulingana na taarifa zilizopatikana kutoka kituo cha kansa cha Ocean Road kuna visa vipya 42,060 vya wagonjwa wa kansa Tanzania ambapo asilimia kati ya 65 mpaka 70 ya wagonjwa hao ni wanawake. Kansa ya kizazi inaongoza kwa asilimia zaidi ya 35 ya visa vay kansa. Umri wa wagonjwa ni kuanzia miaka 18 mpaka miaka 80 ambapo wagpnjwa wengi ni miaka ya 40 na HPV ndiyo chanzo kikuu kwa asilimia 99.9 ya visa vote. Kansa ya kizazi inaweza kuepukika lakini ni chanzo kikubwa cha vifo kwa wanawake nchini Tanzania. Pia, asilimia zaidi ya 80 ya kesi zinazogundulika ni huwa katika hali ya hatari zaidi kwa sababu ya ukosefu wa elimu ya afya, vipimo na tiba ya kansa.

Event details

Matokeo

1. Kuongeza uhitaji na ulazima wa kupima kansa ya kizazi mapema ili kuwapa nafasi wanawake ili wagundue na kujua afya zao mapema. 2. Kupunguza madhara na vifo vinavyosababishwa na kansa ya kizazi kwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya mapema 3. Maisha ya wanawake yataokolewa kwa kuongezeka kwa huduma za afya kwa kutoa huduma mapema.

Washirika Wetu