NBC Dodoma Marathon imekua nguzo muhimu katika sekta ya afya nchini Tanzania, ikichangia mabadiliko ya maana na ya kudumu, kwa kuzingatia afya ya uzazi na ustawi wa wajamii kiafya. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, mbio hizi zimegeuka kuwa jukwaa lenye nguvu ya kukusanya fedha na kujenga uelewa wa matatizo yanayoikumba jamii yetu ikiwemo saratani ya shingo ya kizazi na uhaba wa wakunga wenye ujuzi wa kutosha nchini. Kupitia msaada wa waendeshaji, washirika, na wadhamini, tumefanikiwa kuleta mabadiliko yanayoonekana katika maeneo kama vile uhamasishaji dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, uchunguzi, matibabu, na huduma za afya ya uzazi. Katika mwaka 2025, tunajivunia kupanua dhamira yetu zaidi. Mwaka huu, tunashughulikia hitaji la lililoko katika jamii yetu ambalo mara nyingi huwa halionekani —huduma maalum kwa watoto wenye changamoto ya maendeleo ya kiukuaji, ikiwemo usonji na ugonjwa wa Down (Down Syndrome). Kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamin Mkapa na Wizara ya Afya, tunanzisha ufadhili wa masomo kwa wauguzi wa huduma maalum, tukisaidia kuziba pengo lililodumu kwa muda mrefu katika mfumo wa afya wa Tanzania kwa kuwaandaa wataalamu waweze kutoa huduma zenye wito na utambuzi kwa watoto wenye mahitaji maalum. Ahadi yetu ya kuimarisha afya ya uzazi ina nguvu zaidi sasa kuliko wakati wowote. Tunaendelea kutoa ufadhili wa masomo ya afya ya uzazi ili kuboresha ujuzi wa wakunga na kuimarisha huduma za afya ya uzazi, kuhakikisha kwamba akina mama wengi na watoto wachanga wanapata huduma bora wanazostahili. Kutoka ndani ya kiini chake, NBC Dodoma Marathon ni zaidi ya mashindano ya mbio —ni harakati ya kitaifa ya kujenga mustakabali mzuri wa afya. Kwa kuwekeza katika watu, ujuzi, na uelewa, tunauunda mfumo wa afya unaowahudumia vyema wanawake, watoto, na familia kote Tanzania.
0
Siku0
Saa0
Dakika0
SekundeNBC Dodoma Marathon
Angalia Video